Mwandishi wa kitabu cha TIMIZA MALENGO YAKO, Joel Nanauka
(Kulia) akiwa na mmoja wa watu waliohudhuria kwenye uzinduzi
Imeelezwa kwamba watu wengi wamekuwa wakishindwa kufanikiwa kimaisha
kutokana na kutokuwa na mipango ya kimaisha ambayo wanaweza kuifanyia kazi ili
waweze kufanikiwa kama jinsi ilivyo kwa baadhi ya watu ambao wanaonekana kuwa
na mafanikio.
Hayo
yamesemwa na Mwandishi wa kitabu cha TIMIZA MALENGO YAKO, Joel Nanauka wakati
wa uzinduzi wa kitabu hcho ambacho kinnaelezea mbinu 60 ambazo zinatumiwa na watu
waliofanikiwa kimaisha kuweza kufikia alengo ambayo wamejiwekeakatika maisha
yao.
Nanauka alisema watu wengi wamekuwa
wakitamani kufanikiwa lakini wamekuwa hawajui ni hatua gani za kupitia na
kufanikiwa na baada ya yeye kufanya utafiti wa muda mrefu kwa watu mbalimbali
duniani waliofanikiwa na wasiofanikiwa, ameweza kupata mbinu 60 ambazo ndiyo
zinatofautisha watu wa matabaka hayo mawili
Alisema
kupitia kitabu hicho msmaji ataweza kufahamu ni mambo gani anatakiwa kufanya na
yapi hatakiwi kufanya ili kufanikiwa kama wengine kwa kuzingatia mbinu ambazo
pia zimekuwa zikitumiwa na watu waliofanikiwa katika nyanja mbalimbali kama
biashara, michezo, sanaa na hata uongozi.
“Watu wengi wanapenda kufanikiwa
lakini kama huna malengo huwezi kufanikiwa, watu wengi hawajui wanatumia njia
gani ili kufanikiwa na hadi wanaondoka duniani wanaondoka na ndoto walizokuwa
nazo, ndoto ambazo zilitakiwa kubaki zikifanya kazi duniani,
“Sababu ya kuandika kitabu hiki
ilianza nipotaka kujua utofauti wa waliofanikiwa na wasiofanikiwa,
aliyefanikiwa kwa aliye Marekani na Tanzania na asiefanikiwa aliye Tanzania a
Mareani, nilianza kusoa kwanini wengine wanaweza kufanikiwa katikati ya
mamilioni ya watu na baada ya kupata mawazo ya jumla ndiyo nikapata mbinu 60
ambazo zipo katika kitabu cha TIMIZA AHADI YAKO,” alisema Nanauka.
Nanauka alisema kitabu hicho
kitakuwa kikuzwa kwa Tsh. 10,000 na anaamini kila ambaye ataweza kusoma kitabu
hicho ataweza kupata kitu kipya ambacho kitaweza kumsadiakufanikiwa na kufika
ndoto abazo anatamani kuzifikia.
“Matumaini yangu kila atakaesoma
kitabu hiki maisha yake yabadilike kutokana na mambo ambayo atayasoma na kila
mtu hatajutia kusoma kitabu hiki, nimekiandaa kwa muda mrefu kwa kufanya tafiti
nyingi na kuweka mifano ambayo naamini itabadili maisha ya watu wengi
wataokisoma,” alisema Nanauka.
No comments:
Post a Comment