MAMBO MATANO {5} USIYOYAFAHAMU KUHUSU BAHARI - OREST NGOWI

Breaking

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Friday 7 October 2016

MAMBO MATANO {5} USIYOYAFAHAMU KUHUSU BAHARI

   
Leo ningependa kutoa elimu ndogo kuhusiana na mambo mbali mbali ya husinayo na BAHARI.  Nimeona si busara kukaa na elimu hii ndogo ya JOGRAFIA  pasipo kuwapa na ninyi ili mpate kuwafundisha na wengine.
Mimi naitwa Mwalimu FREDRICK DIDAS PETER KISALALA.  {Rick} 
Leo ningependa tujifunze mambo machache yahusuyo BAHARI.  Najua wengi mmekuwa mkiitazama bahari kwa jicho la kawaida tu,  pasipo kujua mambo yake kwa undani.  Haya ni mambo machache yahusuyo bahari, ambayo naamini kabisa wengi wenu hamuyafahamu.  

1.MPAKA SASA BAHARI IMECHUNGUZWA KWA ASILIMIA 5 TU.  
Hili najua ni jambo la kushangaza kidogo ila huo ndo ukweli.  Kumekuwa na wanasayansi kutoka nchi mbalimbali wakifanya uchunguzi kuhusiana na Baharu,  lakini pamoja na wingi wao huo huo wameweza kuchunguza asilimia 5% tu ya Bahari.  Hivyo wamebakiza asilimia 95%,  kumbe kunaweza kuwa na mengi tusiyo yajua kuhusiana na bahari.

 2. UNAPOMEZA MILILITA  MOJA YA MAJI YA BAHARI,  UNAKUWA UMEMEZA BAKTERIA MILIONI MOJA {1000, 000},  NA VIRUSI MILIONI KUMI {10000000}. 
Hili linaweza kukushangaza kidogo,  ila huo ndiyo ukweli.  Kuna viumbe vingi kwenye maji ya bahari ambavyo huwezi kuviona kwa macho, vikiwemo Bakteria na Virusi. Pamoja na uwepo wa Bakteria n virusi hivyo lakini vingi havin madhara kwa binadamu. 
3.  BAHARI MBILI ZINAPOKUTANA KAMWE HUTOONA MAJI YAKE YAKICHANGANYIKA.  
Huu ni ukweli mwingine usio ufahamu kuhusu bahari.  Kila bahari ina maji yenye tabia tofauti ukilinganisha na mengine,  hivyo pindi maji ya bahari hizi yanapokutana maji yake hujitenegenezea mipaka yenyewe na hayachangani.  Unahitaji kujua ni kwanini?  Subili kwenye masomo yajayo. 

4.  CHINI YA BAHARI KUNA MITO NA MAPOROMOKO YA MAJI.  
Kama ilivyo kwenye nchi kavu,  vivyo hivyo chini ya bahari kuna Mito mikubwa tu yenye kina cha kufikia futi 65 na urefu wa kufikia kilometa 100.  

5.  PAMOJA NA KINA CHA BAHARI KUFIKA HADI FUTI 12400 LAKINI MWANGA HUPENYA KWA FUTI 330 TU.  
Kutokana na ukweli huo,  asilimia kubwa ya bahari hubaki kuwa giza.  
HAYA NI BAADHI TU YA MAMBO USIYO YAFAHAMU KUHUSIANA NA BAHARI.  
Kama una maoni,  au chochote cha kuongezea,  weka comment yako hapa.  Pia tunapokea maswali.  Wanafunzi wanaopenda kujifunza zaidi somo la Geography na History kwa njia ya mtandano wawasiliane nasi kupitia namba hizi 0718 250809 .  Asanteni sana.  

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here