Spika wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Job Ndugai amefanya mabadiliko makubwa kwenye Kamati ya
Bunge ya masuala ya Ukimwi, akiwabadilisha wabunge ishirini na wanne waliokuwa
wanaunda kamati hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa
na Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano cha Ofisi ya Bunge, Ndugai ameteua
wajumbe wapya kumi na sita wa kamati hiyo ambao pia watakuwa wajumbe wa kamati
nyingine.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa Spika
ametumia Mamlaka aliyonayo kikatiba kuunda Kamati za Bunge kadri anavyoona
inafaa, na kwamba mabadiliko haya yamelenga katika kuboresha utekelezaji wa
majukumu ya kibunge.
“Kanuni ya 116 (3) –(5) ya Kanuni
za Kudumu za Bunge, Toleo la Januari 2016 inampa Spika mamlaka ya kuteua
wajumbe ili wawe wajumbe katika kamati mbalimbali za Bunge ikiwa ni pamoja na
mamlaka ya kuongeza, kubadilisha au hata kupunguza idadi ya wabunge katika
kamati za kudumu za Bunge,” imeeleza taarifa hiyo.
Mabadiliko hayo yameanza mara moja
kuanzia mwezi huu wa Oktoba na kwamba wajumbe wote wameshatumiwa barua tayari
kwa maandalizi ya kukutana na kuwachagua viongozi wa kamati hiyo.
Hii ni orodha ya waliokuwa wajumbe
wa kamati hiyo na kamati walizohamishiwa kufuatia mabadiliko hayo:
No comments:
Post a Comment