
Mashahidi wa pande zote mbili
katika kesi ya kupinga ushindi wa Ester Bulaya katika uchaguzi wa mbunge wa
Jimbo la Bunda wamepunguzwa na kuweka mazingira ya shauri hilo kutolewa uamuzi
mapema.
Katika kesi hiyo iliyo Mahakama
Kuu, Bulaya ataanza kujitetea kwa kuita shahidi mmoja baada ya shahidi wa tatu
wa upande wa wawasilisha maombi, Steven Wasira kumaliza kutoa ushahidi juzi.
Upande wa Bulaya, ambaye aligombea
kwa tiketi ya Chadema na kumbwaga mwanasiasa mzoefu, Steven Wasira, umedai kuwa
umeamua kubakia na shahidi mmoja kutokana na waliowasilisha maombi kuwa na
ushahidi dhaifu.
Wakati wajibu maombi wakisema hayo,
upande wa wanaopinga ushindi wa Bulaya wametangaza kufunga ushahidi baada ya
kuita mahakamani mashahidi watatu pekee tofauti na maelezo ya awali kuwa
wangeita watu 15.
Mwanasheria wa Chadema, Tundu Lissu
anayemwakilisha Bulaya ambaye ni mdaiwa wa kwanza katika shauri hilo namba moja
la mwaka 2015, aliieleza mahakama kuwa anakusudia kuita mahakamani shahidi
mmoja.
“Ingawa ushahidi uliowasilishwa
mahakamani na upande wa waleta maombi ni dhaifu na hauna nguvu kisheria kiasi
cha awali tufikiria kutoita shahidi, tumeona ni vyema kuita shahidi mmoja
kujenga hoja zetu za kuishawishi mahakama kutupilia mbali shauri hili,” alisema
Lissu.
Maelezo hayo ya Lissu ni tofauti na
yale aliyoyatoa juzi wakati shauri hilo lilipoahirishwa kwamba asingeita
shahidi yeyote kutokana na ushahidi wa wadai kuwa dhaifu na kukosa mashiko
mbele ya macho ya sheria.
Waliowasilisha maombi ya kutaka
matokeo hayo ya ubunge yatenguliwe ni Magambo Masato, Matwiga Matwiga, Janes
Ezekiel na Ascetic Malagila ambao ni wapigakura wa Bunda.
Wakili anayewakilisha
waliowasilisha maombi hayo, Constantine Mutalemwa amesema wameamua kufunga
ushahidi baada ya kuridhika na ushahidi ambao umeshatolewa na mashahidi
watatu.
Awali, wakili huyo aliieleza mahakama kuwa upande huo ungeita mashahidi 15 kabla ya kurekebisha orodha hiyo na kubakiza 12.
Awali, wakili huyo aliieleza mahakama kuwa upande huo ungeita mashahidi 15 kabla ya kurekebisha orodha hiyo na kubakiza 12.
Wakili Angela Kushagala
anayemwakilisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali na msimamizi wa uchaguzi ambao ni
wajibu maombi namba mbili na tatu, aliieleza mahakama kuwa wanakusudia kuita
mashahidi wawili.
Wakati huohuo, Lissu ameiomba
mahakama kuondoa ombi lao la awali la kutoendelea na usikilizwaji wa shauri
hilo tofauti na awali walipotaka ilitupilie mbali kwa madai kuwa hakuna kesi ya
kujibu.
Lissu alisema upande wa utetezi umepitia upya maombi yao na kugundua kuwa upo uwezekano wa shauri hilo kuchukua muda mrefu iwapo wataendelea kushikilia msimamo wao wa kutaka litupwe.
Lissu alisema upande wa utetezi umepitia upya maombi yao na kugundua kuwa upo uwezekano wa shauri hilo kuchukua muda mrefu iwapo wataendelea kushikilia msimamo wao wa kutaka litupwe.

No comments:
Post a Comment