Master J amedai kuwa inamuuma mno pale ambapo anapoona washindi wa Bongo
Star Search wakishindwa kufanya vizuri tofauti na matarajio.
Akiongea
na mtangazaji wa Jembe FM, JJ, mtayarishaji huyo mkongwe wa muziki, amedai kuwa
sababu kubwa ya washindi hao kushindwa kufanya vizuri ni vipaumbele
wanavyoviwekwa baada ya kushinda.
Amedai kuwa washindi wengi
walipopata fedha zao, walikuwa hawaendi kuwekeza kwenye muziki bali kuzitumia
fedha hizo kutatua changamoto zao za kimaisha.
“Sisi tuliassume tu kwamba
ukimwezesha ataenda kujiwezesha kwenye fani hii ambayo amekuja kutuomba
tumsaidie kwenye BSS. Lakini wengi wamekuwa wananidisappoint sana, wanawekeza
zaidi kwenye vitu vya anasa. Kwahiyo mtu amepata milioni 50 cha kwanza
anafikiria gari, wanafikiria nguo na starehe hizi za vijana,” amesema.
“Hizo hela bwana unatakiwa usifanye
vitu kama hivyo, unatakiwa kuiwekeza kwanza, tumekupatia mtaji, hutakiwi kula
mtaji, mtaji unawekeza, pale unapopata faida ndio unabadilisha maisha yako,”
aliongeza.
Master J amesisitiza kuwa
alimshauri Madam Rita kuwa siku za usoni ni vyema washindi wakapewa fedha nusu
na zingine zikatumika kama mtaji wa muziki wao.
Hadi sasa mshindi wa BSS mwaka jana
Kanumba hajaonesha kufanya vizuri kwenye muziki.
No comments:
Post a Comment