Wakazi wawili wa Manispaa ya
Kinondoni wanashikiliwa na Polisi wakituhumiwa kukutwa na miundombinu ya
Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) yenye thamani ya Sh milioni 61.
Walikutwa na miundombinu ya shirika
hilo ikiwemo vifaa kwa ajili ya kuunganishia umeme.
Akizungumza Dar es Salaam jana,
Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lucas Mkondya, alisema
watuhumiwa hao walikamatwa juzi saa 10 jioni katika maeneo tofauti ya manispaa
hiyo.
Alisema katika tukio la kwanza,
maeneo ya Makumbusho, polisi wakishirikiana na kikosi kazi cha kuzuia uharibifu
wa miundombinu ya Tanesco, walipata taarifa kutoka kwa raia wema kuhusu kuwepo
kwa watu wanaohujumu miundombinu ya shirika hilo.
“Kikosi kazi walifika eneo hilo
katika nyumba ya Wilfred Baruti (45) mkazi wa Makumbusho na kufanya upekuzi
katika nyumba hiyo na vilipatikana vifaa mbalimbali vinavyotumika kuunganisha
umeme vya Tanesco,” alisema Mkondya.
Aidha, alisema pia polisi
walikwenda katika nyumba nyingine ya Beatrice Emmanuel (42) mkazi wa Salasala
Mabanda Mengi walikofanya upekuzi na kufanikiwa kukamata vifaa ambavyo ni nyaya
aina ya drums mbili, rola ya nyaya aina ya AICC ya umeme wa milimeta 50 ambazo
hutumiwa na Tanesco kituo cha Kilimahewa cha Kawe, wilayani Kinondoni.
Mkuu wa kitengo cha mawasiliano Leila Muhaji akizungumza na waandishi wa
kuhusu wizi huo wa vifaa vya umeme vyenye thamani ya milioni 61,Kulia ni Kaimu
Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Lucas Mkondya
No comments:
Post a Comment