Mgombea urais wa chama cha Republican alikuwa anahojiwa na Bw Bush miaka kumi iliyopita alipotoa matamshi ya kudhalilisha kuhusu wanawake.
Ukanda wa mahojiano hayo yaliyofanyika mwaka 2005 ulifichuliwa
majuzi na gazeti la Washington Post.
Baada ya kufichuliwa kwa ukanda huo, viongozi wengi wakuu wa
chama cha Republican walijitenga na Bw Trump ambayo yamezua utata.
Kwenye video hiyo, Bw Bush anasikika akicheka baada ya matamshi
ya Bw Trump.
Billy Bush, 45, ambaye ni mpwa wa rais wa zamani George H W
Bush, alikuwa awali amesimamishwa kazi baada ya kufichuliwa kwa video hiyo.
Amekuwa mtangazaji wa kipindi cha Today kwa miezi miwili pekee.
"Ingawa alikuwa mgeni tu katika waandaaji wa kipindi cha
Today, amekuwa na NBC kwa muda mrefu. Tunamtakia kila la heri," shirika la
NBC limesema kupitia taarifa.
Mke wa Donald Trump, Melania, amemshutumu Bw Bush akisema
alimchochea mumewe kusema mambo mabaya kuwahusu wanawake.
Bw Bush mwenyewe aliomba radhi tarehe 7 Oktoba akisema binafsi
pia aliaibishwa na tabia yake alipokuwa akifanya mahojiano hayo.
No comments:
Post a Comment