Amesema hata hivyo kwamba matamshi ambayo
Bw Donald Trump aliyatoa kwenye kanda ya video ya mwaka 2005 kuhusu wanawake
hayakubalini, ingawa amesema hayaonyeshi mwanamume ambaye yeye amemfahamu.
Mgombea huyo wa chama cha
Republican ana makosa ya kushiriki "mazungumzo ya wavulana faraghani"
lakini alichochewa na mtangazaji wa runinga Billy Bush, Bi Trump amesema.
Kanda hiyo ya ivdoe iliwafanya
viongozi wengi wakuu wa chama cha Republican kuacha kumuunga mkono.
Kwenye video hiyo, Bw Trump
anaonekana akimwambua Bw Bush, ambaye alikuwa mtangazaji wa kipindi cha Access
Hollywood cha NBC, kwamba anaweza kujilazimisha kimapenzi kwa wanawake kwa
sababu yeye ni nyota.
Tangu kutolewa kwa kanda hiyo,
wanawake kadha wamejitokeza na kudai Bw Trump alidhalilisha kimapenzi, madai
ambayo mgombea huyo amekanusha.
"Najua yeye huwaheshimu
wanawake lakini anajitetea kwa sababu yanayosemwa ni uongo," Bi Trump
amesema kwenye mahojiano na CNN.
"Namwamini mume wangu,"
amesema.
"Mume wangu ni mkarimu na
mwanamume mstaarabu. Hawezi kufanya hayo."
Amedai kashta hiyo "imepangwa
na kuandaliwa ili kumzuia kushinda" na kundi la kampeni la mpinzani wake
Hillary Clinton na wanahabari.
"Kwa maelezo waliyopata
(wanahabari) hawafanyi uchunguzi zaidi kuhusu wanawake hawa? Hawana maelezo ya
kweli," ameongeza.
Akiongea kwa mara ya kwanza tangu
madai hayo kutokea, Bi Trump amesema mumewe hajawahi kuwadhalilisha wanawake.
Anasema mara kwa mara wanawake walimwendea mumewe mbele
yake wakitaka awape namba yake ya simu kwa njia isiyofaa.
Akiongea kuhusu kanda hiyo ya mwaka
2005 ya Access Hollywood ambay ilitolewa kwa wanahabari siku 10 zilizopita,
amesema: "Nilimwambia mume wangu, wajua, lugha uliyoitumia haikufaa.
Haikubaliki."
"Na nilishangaa kwa sababu
huyo si mwanamume ninayemfahamu."
Bi Trump anaamini Billy Bush, ambaye
alifutwa kazi na NBC kuhusu kanda hiyo, ndiye wa kulaumiwa.
Bw Trump, alisema,
"alihadaiwa, na kupotoshwa na mtangazaji huyo aseme mambo mabaya".
Zimesalia wiki tatu kabla ya
uchaguzi na kura za maoni zinaonesha Bw Trump yuko nyuma mpinzani wake wa Democratic
Hillary Clinton katika majimbo muhimu yanayoshindaniwa.
No comments:
Post a Comment