Hukumu ya kifo ilitekelezwa dhidi ya mwanamfalme huyo Turki bin
Saud al-Kabir katika mji mkuu Riyadh.
Hakuna maelezo zaidi yaliyotolewa kuhusu jinsi alivyouawa,
lakini watu wengi waliohukumiwa kifo huuawa kwa kukatwa shingo.
Mwanamfalme huyo ndiye mtu wa 134 kuuawa baada ya kuhukumiwa
kifo nchini humo, kwa mujibu wa orodha iliyoandaliwa na shirika la habari la
AFP.
Lakini huwa nadra sana kwa watu wa familia ya kifamle kuuawa,
wanahabari wanasema.
Mwanamfalme huyo alikiri kumuua raia huyo mwenzake, wizara ya
mambo ya ndani imesema kupitia taarifa.
Wizara hiyo imewahakikishia raia kwamba serikali imejitolea
"kudumisha usalama na kutekeleza haki".
Taarifa zinasema familia ya marehemu ilikataa malipo ya
kifedha kama fidia ili kutoitisha hukumu ya kifo dhidi ya mwanamfalme huyo.
Kisa kinachofahamika zaidi cha mtu
wa familia ya kifalme kuuawa ni cha Faisal bin Musaid al Saud, aliyemuua mjomba
wake, Mfalme Faisal, mwaka 1975.
Wengi wa wanaouawa Saudi Arabia
hupatikana na makosa ya mauaji au ulanguzi wa dawa.
Watu karibu 50 hata hivyo waliuawa
siku moja Januari kwa tuhuma za ugaidi, akiwemo mhubiri maarufu wa Kishia
Sheikh Nimr al-Nimr.
No comments:
Post a Comment