Amesema Indonesia inaheshimu haki
za binaadamu lakini hakuna msamaha ikifika katika suala la kuwaadhibu wahalifu
wa uovu huo wa kingono.
Indonesia imepitisha sheria
zilizoibua utata mzozo mapema mwezi huu, na kuidhinisha kutumiwa kemikali
kuhasi wanaume na hivyo kusitisha hamu ya ngono kwa wanaotekeleza unajisi.
Sheria hizo zimezusha mjadala mkali
bungeni.
Muungano wa madaktari nchini humo
unasema madaktari wasihusike, kwani mpango huo unakwenda kinyume na maadili ya
kitabibu.
Mpango huo unahusisha kutumia
kemikali kuwahasi wahusika, pasi na kukatwa sehemu za siri.
Rais Widodo amesema "katiba yetu
inaheshimu haki za binadamu, lakini likija suala la uhalifu wa kingono hakuna
namna".
"Tuna nguvu na tutalishikilia
hilo. Tutatoa adhabu kali kwa uhalifu wa kingono."
Ameongeza: "Kwa maoni yangu
... mpango huu wa kemikali iwapo tutaushinikiza, utasaidia kupunguza uhalifu wa
kingono na kumliza anayetekeleza unajisi hatimaye."
Mpango huo utadumu kwa muda gani?
Tuseme mgonjwa atatumia mbinu hiyo kwa miaka mitatu akiwa gerezani, lakini
akitoka anaweza kwenda kwa dadaktari akafanyiwa marekebisho kwa kutumia dawa za
homoni.
Zaidi ya hayo, adhabu hiyo haiwezi
kufanywa ila na dakatri, kwa sababu ni lazima tufuate maadili ya utabibu.
Unapokuwa daktari, unakula kiapo kutowadhuru binadamu.
Ujumbe wangu kwa madakatri wote
Indonesia ni kuwa ili mradi wewe ni daktari huwezi kufanya hivyo hata kama
serikali inasema ni kwa sababu ni kuwaadhibu walawiti.
Ina madhara na ni kinyume na haki
za binaadamu.
Dr Prijo Sidipratomo ni mwenyekiti wa kamati ya maadili ya
utabibu katika muungano wa madaktari Indonesia.
No comments:
Post a Comment