Kwa muda mrefu, producer mkongwe wa Bongo Flava, P-Funk Majani alikuwa
akizungumza nia yake ya kupata wasanii wa kike kwaajili ya kuwasainisha Bongo
Records.
Na
sasa ametangaza kumpata msichana wa kwanza atakayemwagika wino kuwa chini ya
usimamizi wa label yake kongwe. Anaamini kuwa msichana huyo atafanya mambo
makubwa.
“I finally found the perfect female
artist to sign to Bongo Records. She’s gonna take over the music industry by
storm,” ameandika Majani kwenye picha ya msichana huyo aliyoiweka Instagram.
“What do you think, does she rap or
sing,” amehoji.
Hivi karibuni Majani alisema
anatarajia kutambulisha vipaji vipya takriban vinane vitakavyokuwa chini ya
label yake.
No comments:
Post a Comment