Babutale amezijibu shutuma za baadhi ya mashabiki nchini kuwa
wasanii wa WCB wamekuwa wakinunua tuzo.
Akiongea na Prince Ramalove wa Kings FM, Tale alikuwa na maneno
mafupi tu kuwajibu. “Kama ni rahisi na wao wakanunue,” alisema meneja huyo.
Jumamosi iliyopita Diamond na
Harmonize walishinda tuzo za Afrimma zilizofanyika jijini Dallas, Marekani.
Alidai kuwa tuzo hizo ni za
Tanzania nzima na imeonesha jinsi gani mashabiki wako nao pamoja. Amesisitiza
kwa kuwaomba waendelee kuwapigia kura wasanii wote waliotajwa kwenye tuzo za
MTV MAMA wakiwemo wasanii wake wa WCB, Diamond na Raymond.
Wengine ni Alikiba, Navy Kenzo,
Yamoto Band na Vanessa Mdee.
No comments:
Post a Comment