Msanii wa WCB, Raymond, amedai kuwa wakati mwingine
anapofuata sana misingi ya kazi, baadhi ya watu hudhani kuwa anaringa, kitu
ambacho anadai hawezi kuwa nacho.
“Kwa
mfano, ninaweza nikawa misingi yangu ya kazi inaniambia baada ya show inabidi
niingie kwenye gari niwahi hoteli. Shabiki anataka nishuke, nipige picha,
aniombe namba ya simu,” Ray alimweleza Prince Ramalove wa Kings FM.
Anasema mara nyingi hayo ndio mambo aliyoelekezwa kufanya na uongozi unaomsimamia na ni muhimu kufuata.
Anasema mara nyingi hayo ndio mambo aliyoelekezwa kufanya na uongozi unaomsimamia na ni muhimu kufuata.
“Huo ni msingi wa kazi, mtu hawezi
kusema nimemdharau. Sometimes msingi wa kazi unaniambia haitakiwi nipokee simu
ya interview ama simu ya promota akitaka show, anatakiwa apokee meneja,
nitakavyomwambia ongea na meneja mtu ataona namdharau, lakini mimi nafuata
msingi wa kazi, at end of the day siwezi kubadilika, nafuata msingi wa kazi
sababu ndio unaonipa hela,”
No comments:
Post a Comment