
Fid Q amesema hatimaye tuzo za muziki wa Hip Hop peke yake zitaanza
kutolewa siku za usoni nchini.
Ameyaongea
hayo na mtangazaji wa Kings FM ya Njombe, Prince Ramalove, Fid amesema kuna
watu wengi wanaoitetea hip hip na wamejipanga kuiandalia tuzo zake.
“Hip hop ni muziki unaopiganiwa na
wengi wanaoipenda, ina wapenzi wake ambao huwatoi. Mwanzo ilikuwa ngumu lakini
siku hizi wamekuwa wengi, waligundua wakaenda mashuleni wakasoma vizuri
wakaajiriwa, wakapata nafasi nzuri za kazi kwahiyo nao wanataka kutumia
position zao kusaidia,” amesema Fid.
Kwa upande mwingine Fid
alizungumzia suala la Profesa Jay kufanya Singeli na kama wimbo wake unaweza
kuingizwa kwenye tuzo hizo.
“Hiyo ni sanaa na hivyo ndivyo
ameona yeye ni sahihi. Unapokuwa kwenye beat ya Singeli na yeye amerap, ile
inakuwa ni rap song sio hip hop,” amesisitiza. “Kwahiyo kwenye tuzo za hip hop
anakuwa hajaqualify, lakini yeye kama mwanahiphop anaqualify kuingia, hiyo ni
aina tu nyingine ya muziki ambayo amefanya

No comments:
Post a Comment