Mkali wa wimbo ‘Aje’ AliKiba amefunguka na kuzungumzia ushiriki wa
watanzania kwenye tuzo za MTV Mama Awards 2016.
Muimbaji
huyo ambaye alikuwa miongoni kati ya wasanii watakaotumbuiza kwenye tuzo hizo
na pia aliwania tuzo ya ‘Best Collaboration’ ya wimbo wa Unconditionally Bae
alioshirikiana na Sauti Sol, amesema watanzania walijitahidi lakini walizidiwa
na wasanii wa nje ndiyo maana wakashindwa kutamba.
“Katika ushindani kuna kushinda na
kushindwa sisi hatusemi kuwa tumeshindwa na naamini Tanzania ina vipaji sana na
kila msanii anajitahidi kufanya kwa uwezo wake ili aweze kufikisha nchi yetu
sehemu nzuri,” AliKiba alikiambia kipindi cha Clouds 360. “Kwasasa muziki wetu
umekuwa kwa kasi sana na unazidi kutanuka. Kwa washindi ambao wameshinda kwenye
tuzo za ‘MTV Mama Awards’ wanastaili kwasababu kazi wamefanya na tumeziona”
Katika hatua nyingine muimbaji huyo
amewataka mashabiki wa muziki wake kukaa makao wa kula kwa ajili ya ujio wa
kolabo yake mpya yakimataifa.
No comments:
Post a Comment