Baada ya mashabiki wa Simba kuvunja
viti vya uwanja wa taifa katika mchezo wa Simba na Yanga uliopigwa
Jumamosi na kumalizika kwa sare ya goli ya moja kwa moja, serikali kupitia kwa
Waziri wa Michezo, Nape Nnauye Imepiga marufuku uwanja wa taifa kutumika
na timu za Yanga na Simba.
Waziri Nape amefanya maamuzi hayo baada ya jana Jumapili kufanya ziara katika uwanja wa taifa kushuhudia uharibifu wa viti uliotokea juzi Jumamosi .
Amesema kutokana na tukio ambalo limejitokeza, kuanzia sasa michezo ya timu hizo haitaruhusiwa kufanyika katika uwanja huo hadi pale ambapo serikali itawaruhusu.
“Uwanja huu hautatumika kwa Yanga
na Simba mpaka pale tutakapoamua vinginevyo hapo baadae, hawatatumia uwanja huu
watafute viwanja vingine, sababu hapa kuna pesa za walipa kodi, kuna pesa za
watanzania.
“Wanaotakiwa kutumia uwanja huu
ukiwa mzuri kama ulivyo ni wengi kuliko Yanga na Simba, wapo wengine ambao ni
wastaarabu wanaweza kutumia uwanja huu,” aLIsema Waziri
Nape.
Maamuzi mengine ni Simba kutakiwa
kulipia gharama ya viti 1,781 vilivyoharibika, Simba haitapata mgao wa mchezo
hadi walipe gharama za uharibifu, kamera za CCTV zitafungwa uwanja mzima na
Yanga itatakiwa kulipa gharama ya mageti manne ya upande wa mashabiki wake
yaliyovunjwa.
No comments:
Post a Comment