Hitmaker wa ‘Lover Boy’ Barnaba amewataka wasanii wanaofanya muziki kwa
kubahatisha wabadilike au watafute kazi nyingine.
Muimbaji
huyo amekiambia kipindi cha Dj Show cha Radio One kuwa muziki unapoelekea kwa
sasa ni mgumu na hakuna shabiki anayeweza kuongopewa kwa kuwa wanafahamu
anafanya muziki mzuri na anayebahatisha.
“Wajitathimini wale wanaofanya
muziki mzuri na muziki mbovu, wale wanaofanya muziki mzuri waongeze tu
creativity. Wale wanaofanya muziki ambao hauishi nawashauri waache tu kwa
sababu dunia tunayoenda hakuna ‘uongo uongo’ na mashabiki wanajua nani anafanya
vizuri na nani anafanya vibaya na hakuna wakumdanganya utakuwa unajidanganya
mwenyewe. Nashauri kila mtu aendelee kujituma hakuna uongo, hakuna mtu
anayefanya uongo, hakuna mtu anayetaka kuongopewa,”amesema Barnaba.
Barnaba ameongeza kuwa wasanii
waache kupoteza muda mwingi kwenye kutengeneza video pekee wafanye hivyo mpaka
kwenye audio kuhakikisha zinakuwa nzuri pia.
No comments:
Post a Comment