Producer mwenye mchango mkubwa katika mapinduzi ya Bongo Flava, P-Funk
Majani anasema ‘mwenye muziki wake anarudi.’ Na kwakuwa tunajua ni hits nyingi
kiasi gani zilizotoka kwenye studio yake ya Bongo Records, hiyo si kauli
tunayoweza kuitilia mashaka.
Miezi
ya hivi karibuni Majani ameonekana kutumia muda mwingi zaidi kwenye studio yake
kutengeneza nyimbo mpya. Miongoni mwa kazi anazozipika ni za rapper Cpwaa
ambaye amekuwa kimya kwa takriban miaka miwili na kitu sasa.
Producer huyo ameapa kumrudisha
tena kwenye chati rapper huyo aliyewahi kuhit na nyimbo kama Problem, 6 In The
Morning, Action na zingine.
“Day 2 @cpwaa nailed it! This boy
got No chill, I am bringing him back! Stay tuned #BongoRecords #DreamBig
#KiumeniSoundTracks #MwenyeMzikiWakeAmerudi,” aliandika Majani kwenye Instagram
hivi karibuni.
Naye Cpwaa amemuelezea Majani kama
kaka na mwalimu wake na kwamba kufanya kazi naye tena ni heshima kubwa. “Again
it was a good day! #BongoRecords PFunk @majani187
#TheGodFatherOfBongoFlavaMusic is more than a Music Producer! He is a Mentor, a
Brother, and Family. Before the session we went through a lot of ongoing main
stream shiit, this brother is doing his homework.i keep learning everyday from
him #Discpline is number 1thing when it comes to work with
him.#TheComeBackOfCpwaa.”
No comments:
Post a Comment