Rapper Kanye West amelazwa katika hospitali huko jijini Los Angeles.
Hatua hiyo imekuja baada ya kukatisha show zilizokuwa zimesalia za ziara yake
ya Saint Pablo kutokana na kukabiliwa na uchovu.
Kwa
mujibu wa NBC News, Kanye alipelekwa hospitali baada ya polisi kupigiwa simu ya
dharura. Wiki hii rapper huyo ametengeneza vichwa vya habari kwa kauli tata
alizozitoa wakati wa show zake mbili zilizopita ikiwemo kuwadiss Jay Z na
Beyonce na kumfagilia Donald Trump.
Kutokana na kukatisha show
zilizokuwa zimesalia, West atapata hasara ya zaidi ya dola milioni 10.
Familia yake ipo kwenye wakati
mgumu kwa sasa. Mwezi uliopita, mkewe Kim Kardashian, alivamiwa kwa mtutu wa
bunduki na kuporwa mali huko Paris, Ufaransa.
No comments:
Post a Comment