Kufuatia kifo cha aliyekuwa Spika
wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanza nia (2005-2010), Samuel Sitta, mwanae
wa kiume ameweka wazi maneno matatu ya mwisho aliyoyatamka, yenye maana nzito
katika maisha.
Akizungumza nyumbani kwa marehemu,
Meya wa Kinondoni, Benjamini Sitta ambaye ni mtoto wa kiume wa marehemu,
alisema kuwa baba yake alitoa maneno matatu ya kuukubali ukweli wa maisha baada
ya Daktari kumueleza kuwa asingeweza kupona.
“That’s life (hayo ndiyo maisha),” Benjamin
alikariri maneno ya baba yake. Alisema hayo yalikuwa maneno yake ya mwisho
baada ya kuelezwa ukweli na daktari wa hospitali ya Technical University of
Munich nchini Ujerumani alipokuwa akipatiwa matibabu.
Maneo ya Sitta ni funzo kubwa kwa
watu wote kuwa maisha huanza na huisha, hiyo ndiyo maana ya maisha na hakuna
aishie milele hivyo tuishi kwa kuzingatia maana hiyo ya maisha na kuikubali.
Sitta ambaye anakumbukwa kwa kauli
mbiu yake na matendo ya kusimamia ‘kasi na viwango’, alifariki kutokana na
ugonjwa wa tezi dume uliokuwa ukimsumbua kwa muda mrefu.
Alitangaza kustaafu siasa muda
mfupi baada ya kukamilika kwa kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka jana, ambapo
yeye alikuwa mmoja kati ya waliokuwa msitari wa mbele kumnadi mgombea urais wa
Chama Cha Mapinduzi, Dkt. John Magufuli aliyeshinda uchaguzi huo.
Benjamini alieleza kuwa marehemu
atazikwa Urambo Mkoani Tabora na kwamba ratiba ya mazishi itatolewa na Ofisi ya
Bunge ambayo ndiyo inayoratibu mazishi
“Tumempoteza baba na kiongozi
ambaye tulikuwa tunamtegemea kwa ushauri na masuala mbalimbali, tutafuata yale
aliyokuwa akituelekeza,”alisema Benjamini.
Hakika Taifa limempoteza mtu
muhimu, pengo lake halitazibika kamwe. Bwana alitoa, Bwana ametwaa, jina lake
lihimidiwe!
No comments:
Post a Comment