Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari
Tanzania (TPA) imepokea boti mbili za kisasa za kuhudumia meli kutoka China
zitakazotumika katika Bandari za Dar es Salaam na Tanga.
Meneja Mawasiliano wa TPA,
Janeth Ruzangi alisema ujio wa boti hizo zilizopolewa jana utasaidia kuongeza
kasi ya utendaji kazi na ufanisi katika bandari hizo.
Alisema ujio wa boti hizo ni sehemu
ya mkakati wa TPA kuongeza vitendea kazi kwa upande wa majini na nchi kavu ili
kuongeza kasi ya upakuaji na upakiaji wa mizigo kwa kiwango cha kimataifa na
hivyo kuvutia wateja wengi.
Nahodha Mkuu wa TPA, Kapteni
Abdullah Mwingamno alisema boti ya tani 70 iliyopewa jina la Valeria
Rugaihuruza itabaki Dar es Salaam kwa ajili ya kuhudumia meli zinazoshusha
mafuta katika Boya la SPM lililopo Mji Mwema, wakati nyingine inayoitwa
Mwambani itapelekwa Bandari ya Tanga kwa ajili ya kuhudumia matishari.
Boti ya MV Valeria Rugaihuruza
imeundwa na ‘crane’ yake pamoja na boti nyingine ndogo mbili ndani yake kwa
ajili ya kusaidia utendaji kazi kwenye boya la mafuta. Boti ya MV Mwambani ina
uwezo wa kuvuta tishari lenye uwezo wa kubeba tani 3,500 za mizigo.
No comments:
Post a Comment