Naibu Kamishna mstaafu wa Magereza
nchini (DCP), Luhusa Chiza (62) amefariki dunia katika mazingira ya utata
kwenye Hoteli ya Kitemba mjini Dodoma.
Kwa mujibu wa mashuhuda tukio hilo,
mwili wa Chiza uligunduliwa juzi mchana na mmoja wa wahudumu wa hoteli hiyo
alipotaka kufanya usafi.
Taarifa zaidi kutoka ndani ya hoteli hiyo iliyopo Barabara ya Sita katikati ya mji, zilidai Chiza aliingia Novemba 15 usiku na msichana ambaye alitoroka baadaye.
Taarifa zaidi kutoka ndani ya hoteli hiyo iliyopo Barabara ya Sita katikati ya mji, zilidai Chiza aliingia Novemba 15 usiku na msichana ambaye alitoroka baadaye.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma,
Lazaro Mambosasa alisema mwili wa Chiza ulikutwa ukiwa na damu puani na kwamba,
aliingia chumbani akiwa na msichana ambaye wanamtafuta.
Alisema kamishna huyo alifika mjini
hapa akitokea jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kukagua viwanja vyake na
kwamba, alikuwa akielekea mkoani Kigoma.
Meneja wa Hoteli ya Kitemba, Crispin Daniel alisema mteja huyo aliingia Novemba 15.
Meneja wa Hoteli ya Kitemba, Crispin Daniel alisema mteja huyo aliingia Novemba 15.
“Mhudumu alikuja kuniambia kuna
mteja hajisikii vizuri chumbani, anatapika si kwamba alifariki dunia akiwa
hapa. Ingekuwa hivyo usingekuta hivi,” alisema.
Alisema baada ya kupokea maelezo
hayo, alipiga simu polisi na walifika na kumchukua na hafahamu
kilichoendelea.
“Watu wanasema alifia hapa kwa
sababu waliona polisi wamejaa, ukweli alitoka akiwa anaumwa ndicho
ninachofahamu,” alisema.
Kaimu Mfawidhi wa Hospitali ya
Rufaa ya Dodoma, Dk Caroline Damian alithibitisha kupokewa kwa mwili huo juzi
mchana.
“Tayari tumeshamfanyia postmortem
(uchunguzi) na tumechukuwa sampuli ya chakula, kwa ajili ya kupeleka kwa Mkemia
Mkuu wa Serikali,” alisema.
Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dodoma,
Antonio Kilumbi alisema mwili wa ofisa huyo ulisafirishwa jana kwenda Wilaya ya
Kasulu mkoani Kigoma kwa mazishi.
“Alikuwa akitokea Dar es Salaam kuchunguza afya yake maana anapressure (shinikizo la damu) na alishawahi kuzimia mara nyingi tu,”alisema Kilumbi.
“Alikuwa akitokea Dar es Salaam kuchunguza afya yake maana anapressure (shinikizo la damu) na alishawahi kuzimia mara nyingi tu,”alisema Kilumbi.
No comments:
Post a Comment