Mchezaji wa Klabu ya Montreal Impact Didier Drogba usiku wa kuamkia leo
timu yake imeibuka na ushindi wa 3-2 dhidi ya Toronto FC kwenye fainali ya ukanda
wa mashariki.
Baada
ya mchezo huo wa kwanza wa fainali ya ukanda wa mashariki kumalizika, Drogba
aliwaambia waandishi kuwa huo ndio ulikuwa ni mchezo wake wa mwisho kwenye
uwanja wa nyumbani wa Montreal.
“Bado kuna mechi 1 au 2 zilizobaki.
Mechi ya wiki ijayo ni muhimu sana.
Kila mmoja anafahamu kuwa hii
ilikuwa mechi yangu ya mwisho hapa (Uwanja wa nyumbani). Sasa acha tuelekeze
akili zetu katika nusu fainali.” amesema Drogba.
Mshindi wa nusu fainali hiyo
atacheza mechi ya fainali ambayo itapigwa Disemba 10.
Drogba ambaye amejiunga na klabu
hiyo Montreal Impact mwaka 2015 akitokea Chelsea, na kufanikiwa kucheza mechi
33 akifunga goli 27 kunako timu hiyo inayoshiriki MLS.
No comments:
Post a Comment