Wachezaji wa timu ya taifa ya Argentina wamegomea kuongea na
wanahabari wakiongozwa na nahodha wa timu hiyo Lionel Messi amewaongoza
wachezaji wenzake kususia kuongea na wanahabari baada ya ukosoaji kuhusu
uchezaji duni wa timu hiyo.
Messi,
29, alitangaza mgomo huo baada yake kufunga bao wakati wa ushindi wao wa 3-0
mechi ya kufuzu kwa Kombe la Dunia dhidi ya Colombia.
Kituo kimoja cha redio kilikuwa
kimeripoti kuwa mshambuliaji Ezequiel Lavezzi alivuta bangi baada ya kipindi
cha mazoezi, tuhuma ambazo amekanusha.
“Tumepata tuhuma nyingi, kukosewa
heshina na hatujasema lolote,” messi alisema.
Messi na wenzake 25 waliondoka kutoka kwenye kikao na wanahabari bila kuzungumza nao baada ya mechi hiyo dhidi ya Colombia.
Messi na wenzake 25 waliondoka kutoka kwenye kikao na wanahabari bila kuzungumza nao baada ya mechi hiyo dhidi ya Colombia.
Taarifa zinasema Lavezzi
atakishtaki kituo hicho cha redio.
“Tunajua wengi wenu ambao hamna
heshima kwa mchezo huu, lakini kuingilia maisha ya kibinafsi ya mtu mmezidi,”
Messi aliongeza.
Argentina walikosolea sana baada yao kulazwa 3-0 na Brazil lakini ushindi wao dhidi ya Colombia umewawezesha kupaa hadi nambari tano na kwenye nafasi za kushindania kufuzu kwa Kombe la Dunia.
Argentina walikosolea sana baada yao kulazwa 3-0 na Brazil lakini ushindi wao dhidi ya Colombia umewawezesha kupaa hadi nambari tano na kwenye nafasi za kushindania kufuzu kwa Kombe la Dunia.
Mataifa manne yanayomaliza juu
kanda ya Amerika Kusini hufuzu moja kwa moja. Nambari tano hukutana na mpinzani
kutoka bara jingine kuamua mshindi.
No comments:
Post a Comment