Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mbeya, imemhukumu mtoto wa Mbunge wa
Mbarali, Haroon Mulla Pirmohamed (CCM) kulipa faini ya Sh138,390,000 au kifungo
cha miaka 20 jela, baada ya kukiri kosa na kutiwa hatiani kwa kumiliki nyara
mbalimbali za Serikali.
Katika
kesi hiyo, mtoto huyo Pirmohamed Haroon alikutwa akimiliki kilo 46 za nyama ya
tandala, mbawala, swala pala, tohe, njiwa pori, kanga pori na pembe za tandala
na tohe vyote vikiwa na thamani ya Sh138,390,000.
Akisoma hukumu, Hakimu Mkazi
Mwandamizi wa Mahakama hiyo, Michael Mteite alimhukumu mshtakiwa huyo kulipa
faini hiyo ambayo ni mara 10 ya thamani ya nyara alizokutwa nazo na iwapo
atashindwa atumikie kifungo cha miaka 20.
Hata hivyo, baada ya kutolewa kwa hukumu hiyo, Haroon
alikwepa adhabu ya kifungo kwa kulipa kiasi hicho cha fedha na kupatiwa risiti
ya malipo ya Serikali namba 8870022.
Source: Mwananchi
Source: Mwananchi
No comments:
Post a Comment