Familia ya Chijoke Stephen Obioha ilifahamishwa kuhusu hatua
hiyo Jumatano.
Obioha alipatikana na kilo 2.6 za bangi Aprili 2007, kiasi
kilichokuwa kimezidi kipimo cha gramu 500 ambacho mara moja humfanya mtu
kuhukumiwa kwa ulanguzi wa dawa za kulevya chini ya sheria za Singapore.
Afisa wa Amnesty International Rafendi Djamin amesema shirika
hilo limeshangazwa na hatua hiyo ya Singapore kumnyima mshtakiwa huyo msamaha.
Hata hivyo, alisema shirika hilo bado lina matumaini kwamba
Singapore haitatekeleza adhabu hiyo "katili na isiyoweza kubatilishwa
dhidi ya mtu huyo aliyehukumiwa kifo kwa kosa ambalo halifai adhabu ya
kifo."
"Hukumu ya kifo si suluhu. Haitaangamiza daw azote za
kulevya Singapore. Kwa kuwanyonga watu kwa makosa ya kuwa na dawa za kulevya,
ambayo hayafikii kiwango cha makosa makubwa ya uhalifu, Singapore inakiuka
sheria za kimataifa.
"Mataifa mengi ulimwenguni yameacha adhabu hii ya kikatili,
kinyama nay a kudunisha."
No comments:
Post a Comment