Serikali kupitia Mamlaka ya
Vitambulisho vya Taifa (NIDA) imesema kuanzia Desemba mwaka huu mpaka Januari
2017 itaanza kutoa namba maalum za utambuzi kwa wananchi.
Mkakati huo umetangazwa jana na
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba alipokutana na uongozi
na wafanyakazi wa NIDA, kwa lengo la kujadili mikakati mbalimbali ya kuboresha
utendaji wa mamlaka hiyo.
Alisema tayari serikali
imekamilisha kanzidata ya wananchi walizozipata kutoka Tume ya Taifa ya
Uchaguzi NEC na kwamba, tayari taasisi zaidi ya 35 zimeanza kutumia taarifa za
NIDA katika kufanya utambuzi wa wafanyakazi wao sawia na kupunguza usumbufu kwa
wananchi kuhusu taarifa zinazowahusu.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa NIDA
Bw. Andrew Massawe alisema kwa zoezi la awali lililofanyika nchi nzima tayari
wamefanya uhakiki wa kuwatambua watumishi wa serikali takribani laki tano na
elfu sitini na tano.
No comments:
Post a Comment