Tanzania imeingia rasmi kwenye
mfumo maalum wa kimataifa wa kupata huduma za afya ya UKIMWI kwa njia ya simu
bila malipo mfumo ambao umefadhiliwa na nchi ya Marekani.
Akizindua mfumo huo Kaimu Balozi wa
Marekani nchini Bi. Virginia Blaser amesema mfumo huo utawafikia zaidi ya watu
laki nane huku lengo kuu la mfumo huo likiwa ni kupunguza maambukizi ya Virusi
vya Ukimwi (VVU) na Ukimwi kutoka asilimia 7.5 mpaka asilimia 5 hadi kufikia
asilimia 0.0.
Amesema watu wote ambao wanadhaniwa
kuwa na maambukizi ya virusi vya Ukimwi hadi kufikia mwaka 2020 wawe tayari
wamepimwa kwa asilimia 90, asilimia 90 waanze kutumia dawa, na asilimia 90
kiwango chao cha maambukizi kiwe kimepungua.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa
Taasisi ya TAYOA nchini Bw . Peter Masika amesema katika ufadhili wa mfumo huo
wao wakiwa ni wasimamizi wa mfumo watahakikisha unawafikia watanzania wote hasa
wale wasiofikiwa na huduma muhimu za kiafya na kuwataka watanzania kujitokeza
kwa wingi kutumia mfumo huo ili kutokomeza ugonjwa wa Ukimwi.
No comments:
Post a Comment