Jeshi la Polisi mkoani Pwani
limezungumzia kifo cha askari wake PC Armand Furaha (33) aliyejipiga risasi
kifuani bila kukusudia na kufariki dunia.
Askari huyo alijipiga risasi hiyo
usiku akiwa anaelekea kwenye lindo nyumbani kwa Mkuu wa Wilaya ya Kibaha.
Tulio hilo lilitokea saa moja usiku
eneo la Mailimoja sokoni usiku wa kuamkia jana, wakati askari huyo akiwa njiani
kuelekea kwenye kituo cha lindo alichopangiwa.
Kaimu Kamanda wa Polisi Pwani,
Blasius Chatanda amesema askari huyo alijipiga risasi bahati mbaya kwa bunduki
aina ya SMG akiwa amekaa kwenye kiti cha mbele katika gari alilokuwa anasafiria
kwenda lindoni.
Amesema uchunguzi wa awali umebaini
kuwa askari huyo alikuwa tayari ameweka risasi chemba kwenye bunduki hiyo
aliyokuwa nayo na kwa bahati mbaya akiwa anashuka kwenye hilo gari ndipo risasi
hiyo ikafyatuka na kumpiga kifuani eneo la kushoto na kufa wakati akipatiwa
matibabu katika Hospitali ya Tumbi.
“Kabla ya tukio hilo, askari huyu
aliwasili kazini jioni na kukuta amepangiwa kituo cha ulinzi kwa mkuu wa wilaya
hivyo kama ilivyo ada alichukua zana za kazi ikiwemo bunduki hiyo na kuanza
safari ya kuelekea lindoni kwake huko kwa DC, lakini bahati mbaya hakufika
alifariki kwa kujipiga risasi bahati mbaya,” amesema Chatanda.
Akizungumzia suala la askari
kujipiga risasi Msemaji wa Jeshi la Polisi, Advera Bulimba amesema kila tukio
hutokana na mazingira tofauti.
No comments:
Post a Comment