Mtoto Adam aliyezungushiwa kaduara akiwa katika cover la wimbo Wanandoto
Video ya wimbo ‘Wanandoto’ ya msanii wa muziki wakufoka, Kala Jeremiah
imefanikisha kurejesha furaha ya familia moja ambayo ilipotelewa na mtoto wao
wa kiume toka September 2015.
Mama
wa mtoto huyo aitwae Adam, alifanikiwa kumuona mwanae huyo kupitia video ya
wimbo huo ambao unazungumzia mazingira magumu wanayopitia watoto yatima.
Akiongea na Bongo5 Jumanne hii, Kala
amesema alipigiwa simu na mama huyo akimuulizi mtoto huyo alimuona kupitia
video yake ya Wanandoto.
“Nilipigiwa simu na mtu
akaniambia Kuna mama kamuona mtoto wake kwenye video yangu ya Wanandoto na
mtoto huyo alipotea tokea mwaka jana mwezi wa 9,” alisema Kala “Mama wa mtoto
alifanya jitihada zote za kumpata mtoto wake bila mafanikio lakini juzi juzi
akiwa anatazama video ya Wanandoto akamuona mwanae kwenye video na kupata
mshangao na mshituko ndipo alipoamua kumtafuta mtangazaji flani wa redio flani
ndipo mtangazaji huyo akanitafuta na kuniunganisha na mama huyo,”
Alilifanua zaidi “Mama yule
alinieleza kwa masikitiko makubwa sana kuwa mtoto wake alipotea toka mwaka jana
mwezi wa 9 alimtafuta Sana kila sehemu alienda kwa waganga wengi alienda kwenye
maombi ya kila aina lakini hakufanikiwa kumpata mwanae.
Mtoto Adamu akiwa na mama yake
Rapa
huyo amesema baada ya kumsikiliza mama huyo aliamua kumwelekeza katika kituo
cha watoto yatiba ambacho kinamlea mtoto huyo.
“Baada ya mama huyo kunieleza yote
hayo nikawasiliana na kituo cha kulelea watoto cha Chakuwama ambapo mtoto Adam
analelewa nikawaeleza habari hii wakakiri kweli Adam yupo na ni kweli walimpata
mwaka jana mwezi wa 9. Basi nikawasiliana tena na mama yake Adam na kumwambia
kuwa nimewasiliana na mlezi wa kituo amekiri kuwepo kwa Adam kituoni hapo na
kwakuwa mimi sipo Dar kwa muda huu nikamuunganisha mama Adam na mlezi wa kituo
kile wakawasiliana na jana mama Adam amefika kituoni pale na kuonana na mwanae
na amefurahi Sana,”
Kwa upande wa mama Adam,
amemshukuru Kala kwa kufanikisha kupatikana kwa mtoto wake.
“Kwa kweli namshukuru Mungu kwa
kufanikiwa kunionyesha mtoto wangu ana mwaka mmoja na miezi miwili toka apotee
na nilitoa taarifa kila sehemu na nikashindwa kumpata. Kwa hiyo naweza kusema
video Kala imerudisha furaha yangu, namshukuru sana,” alisema Mama Adam.
No comments:
Post a Comment