Miss Tanzania 2016 Diana Edward ambaye ndiye mrembo anayetarajiwa kwenda
kuiwakilisha Tanzania kwenye mashindano ya urembo ya dunia ‘Miss World’,
ameilalamikia kamati ya mashindano hayo kwa kumtelekeza hali ambayo amedai
inaweza kumfanya ashindwe kuiwakilista Tanzania katika mashindano hayo.
Mrembo
huyo amedai bado hajapata msaada wowote kutoka katika Kamati ya Miss Tanzania
na serikali, ikiwa zimebaki siku chache kuweza kufikia kwenye mashindano hayo
ya dunia.
“Hata zawadi zangu zilizo haidiwa
sijapewa, kwahiyo inakuwa ngumu kwangu kujiandaa na mashindano ya miss dunia,”
Diana alikiambia kipindi cha Planet Bongo cha EA Radio. “Siku ishirini
zilizobaki ni ndogo natakiwa kuandaa documentary ya historia ya kimasai Arusha.
Sina kitu chochote chakufanyia natakiwa nilipe hiyo, natakiwa nilipe team
support kwa sababu natakiwa kwenda kuonyesha Tanzania yangu, natakiwa kuonyesha
beauty of purpose,”
Aliongeza, “Tanzania, viongozi,
serikai, Miss Tanzania cometee, i need suport, i need what i deserve, unajua
mimi ni mtu ambaye najiongeza, kwa hiyo nikipewa suport kidogo i push it up,
kuna watu ambao nimewaomba suport wamenipa vya kutosha, kwa hiyo i need what i
deserve”
Kwa upande wa afisa uhusiano wa
kamati ya Miss Tanzania, Hidan Rico amesema shughuli za maandalizi ya miss huyo
zinafanywa na Kamati ya Miss Tanzania.
“Hayo mambo yanashughulikuwa na
Kamati ya Miss Tanzania. Yaani ameshaanza kuongea na vyombo vya habari? Mimi
sina mamlaka ya kulijibu hilo la zawadi lakini nachojua maandalizi yake
yanafanyika na kamati,” alisema Rico.
No comments:
Post a Comment