Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo, Mhe. Nape Nnauye
wametoa pole kwa fimilia ya bondia Thomas Mashali aliyeuawa kwa kupigwa baada
ya kupigiwa kelele za mwizi kufuatia ugomvi uliozuka maeneo ya Kimara, jijini
Dar es Salaam.
Akiongea
katika kipindi cha Jahazi Jumatatu hii, Nape amesema tasnia ya michezo
imempoteza mtu muhimu ambaye ametangaza nchi kupitia mapigano mbalimbali.
“Tumesikitishwa sana kifo chake
ambacho kimetokea kikatili, ni jambo ambalo limetushtua sana kwa sababu
tumempoteza mtu muhimu ambaye amefanya kazi kubwa ya kuiwakilisha nchi yetu na
kuendeleza tasnia ya ngumu. Kwa hiyo kwa niaba ya serikali natoa pole kwa rais
wa chama cha mabondia Tanzania, viongozi, ndugu pamoja na jamaa na marafiki
ambao wameguswa kwa namna moja,” alisema Nape.
Mashali aliyezaliwa kwa jina
Christopher Fabian Mashale aliuawa baada ya kupigwa akiwa huko Kimara jijini Dar
es Salaam. Inasemekana wakati akinywa pombe, ulizuka ugomvi na mtu mmoja ambaye
anadaiwa kupiga kelele kusema Mashali ni mwizi na watu kuanza kumshambulia.
No comments:
Post a Comment