Mkurugenzi wa Mkubwa na Wanawe ambaye pia ni diwani wa kata ya Kilungule
Said Fella au Mkubwa Fella, amewataka watu kutambua mchango wake kabla hajafa
badala ya kuponda jitihada zake huku akiwataka watu kuacha kuongea vitu
wasivyovijua.
Fella
ambaye pia ni boss wa Kundi la muziki la Yamoto Band, amesema watu wamekuwa
wanaongoza kumsema vibaya badala ya kumsifia na kumpongeza, kwani kazi
anayoifanya ni kubwa.
“Halafu kuna watu wanasemaga Said
Fella sijui kawafukuza Yamoto, leo Yamoto wapo ndani humu,” Fella alikiambia
kipindi cha Planet Bongo cha EA Radio “Nimekuja kukata midomo domo, kwa sababu
tusiwe tunaongea tu inafika wakati ukweli midomo inaumba, Mkubwa na Wanawe ina
watoto 102, kwa hiyo fella anatengeneza vingi, kuna watu wananikwaza, inatakiwa
hata siku moja na mimi nipewe certificate ya kusaidia mtaa, kila siku
wananibomoa wananibomoa, nisifieni kabla sijafa ninachokifanya hiki”,
Pia Mkubwa Fella alisema anayajua
madai kuwa amewadhulumu Yamoto band, lakini ukweli ni kwamba vijana hao mpaka
sasa kila mmoja ana nyumba yake, kitu ambacho kimetokana na juhudi zake
No comments:
Post a Comment