Ukistaajabu ya Musa utaona ya Firauni. Maafisa wa usalama nchini Ghana
wamewakamata watu watatu kwa kuhusishwa na kuwa na ubalozi bandia wa Marekani
mjini Accra ambao umetumika kuwalaghai raia maelfu ya fedha kwa miaka 10.
Idadi
kamili ya walaghai hao haijabainika, lakini walifumaniwa na polisi wa Ghana
wakisaidiana na maafisa wa usalama wa ubalozi wa Marekani. Kwa sasa
waliokamatwa wanahojiwa ili kuelezea zaidi kuhusu udanganyifu huo.
Genge linalosimamia ubalozi bandia
liliwatafuta wateja kutoka mataifa jirani na ndani ya nchi kisha kuwaleta
kwenye jengo lililokua na bendera ya Marekani.
Kila mteja aliyekata kupata Visa ya
kusafiri Marekani alitozwa dola 6,000. Baadhi ya Visa hata hivyo zilikua
halisi, hali inayozua wasi wasi kwamba huenda walishirikiana na baadhi ya
wafanyikazi wa ubalozi wa Marekani mjini Accra.
Waliokamatwa ni wenyeji na raia wa
Uturuki.Wengi wa wateja waliodanganywa ni wakaazi wa maeneo ya mashambani, na
waliamini ubalozi huo bandia baada ya kukutana na wanachama wa genge hilo
kutoka Uturuki. Ubalozi huo bandia pia haukuwekwa kwenye mtandao na waliwapata
wateja kwa kuzungumza na raia
No comments:
Post a Comment