Msanii wa muziki wa hip hop, Young Dee amesema ameachia wimbo ‘Furaha’
ili kumfariji msanii wenzake Dojo Janja aliyefiwa na Baba yake hivi karibuni.
Rapa
huyo ambaye alikuwa kimya kwenye muziki tangu atangaze kuachana na matumizi ya
Madawa ya kulevya, amedai hakuwa na mpango wa kuachia wimbo huo.
Kupitia Instagram, Dogo Janja
ameandika:
Nilipanga kuachia video yangu nikiwa na furaha sana.
Furaha yangu nilitamani sana itawale kwanzia kwangu, mashabiki wangu, pamoja na
wasanii wenzangu. Bahati mbaya msanii mwenzangu @dogojanjatz amepoteza nguzo
imara sana katika maisha yake. Miaka 8 iliyopita nilipitia changamoto kama hiyo
kwa kumpoteza mzee wangu. Kitu pekee nilichokua nahitaji ni FURAHA itokanayo na
faraja kutoka kwa watu walionizunguka. Nilikua sina mpango wowote wa kuachia
wimbo wangu wiki hii. Lakini nimeamua kuachia Video ya wimbo wangu leo, kama
Dedication kwa @dogojanjatz. Wimbo wangu unaitwa FURAHA. Naamini ni nguzo pekee
anayoihitaji Mwanangu Janjaro kwa sasa. You Have all my Support Young Badman, I
have Nothing But Love to You.
No comments:
Post a Comment