Waziri Mkuu Kassim Majaliwa jana
alifanya ziara ya kushtukiza katika hospitali ya Mkoa ya Mount Meru ambako
kulikuwa na tuhuma za kuibwa watoto, lakini alishuhudia wazazi watatu wakilala
kitanda kimoja.
Ziara hiyo ilitokana na taarifa alizolalamikiwa na wananchi juzi
kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, kwamba
hospitali hiyo ina matukio ya wizi wa watoto wachanga.
Hata hivyo, jana baada ya kufika katika hospitali hiyo, Majaliwa alishuhudia msongamano katika wodi ya wazazi na kuagiza kuboreshwa hospitali za pembezoni.
Majaliwa aliagiza uongozi wa hospitali hiyo kuhakikisha wanaondoa changamoto za ongezeko la wagonjwa na kuboresha huduma katika hospitali hiyo.

Akizungumzia sakata ya kupotea kwa
watoto katika hospitali ya mkoa alivitaka vyombo husika kuendelea na uchunguzi
kwa kuwa suala hilo tayari lipo mikononi mwa vyombo vya dola.
Wiki mbili zilizopita mzazi, Walda Mussa alisema kuwa alijifungua mtoto katika hospitali hiyo lakini hadi alipotoka hakumpata.
Wiki mbili zilizopita mzazi, Walda Mussa alisema kuwa alijifungua mtoto katika hospitali hiyo lakini hadi alipotoka hakumpata.
“Nilikuja hapa hospitali Oktoba 4
na Oktoba 7 nikajifungua kwa upasuaji wakamchukua mtoto na kumpeleka chumba cha
joto, akaja mume wangu akaenda kumuona mtoto mzima, siku ya pili alienda
kumuona mtoto pia akiwa mzima lakini siku ya tatu, tulipokwenda wote mimi na
mume wangu tuliambiwa mtoto alifariki na hatujawahi kuona mwili wake,” alisema mwanamke
huyo hivi karibuni.
Mganga Mkuu mfadhiwi wa hospitali
ya Mkoa Mount Meru, Dk Jackline Urio alipotakiwa kuelezea sakata hilo, alisema
kuwa mtoto huyo baada ya kuzaliwa alifariki dunia na baadaye mwili ulipelekwa
chumba cha kuhifadhi maiti katika hospitali hiyo.
No comments:
Post a Comment