Rais wa Marekani Donald Trump amemfuta kazi kaimu mwanasheria mkuu Sally
Yates saa chache tu baada ya kuwaagiza mawakili wa idara ya haki nchini humo
kutotetea uamuzi wa kuwawekea vikwazo raia wanaotoka katika baadhi ya mataifa
ya kiislamu.
Taarifa ya Ikulu ya
Whitehouse imemshtumu kwa usaliti.
Sally Yates ambaye
aliteuliwa na Obama alisema kuwa hafikirii kwamba marufuku hiyo ya muda kwa
raia wa mataifa saba ya Kiislamu ni halali.
Wadhfa wake
umechukuliwa na kiongozi wa mashtaka katika mahakama ya kijimbo huko Virginia
Dana Boente.
Agizo hilo la rais
lililotiwa saini Ijumaa iliopita limesababisha maandamano nchini Marekani na
ughaibuni.
Awali kundi moja la
wanadiplomasia liliandika barua likikosoa agizo hilo wakisema litazidi
kuhatarisha usalama wa taifa hilo.
No comments:
Post a Comment