Mikoa ya Mwanza na Dar es salaam inatajwa kukabiliwa na changamoto ya
upatikanaji wa huduma za afya ya uzazi na vifo vitokanavyo na utoaji mimba usio
salama, hali inayosababisha wanawake zaidi ya 400,000 kulazimika kutoa mimba
kwa usiri mkubwa kila mwaka huku asilimia 40 kati yao wakiishia kupata matatizo
makubwa ya kiafya.
Akiwasilisha
tathimini ya utekelezaji wa maazimio na mpango kazi wa shughuli za chama cha
wanawake wanasheria tanzania ( TAWLA ) kwa mwaka 2016 juu ya umuhimu wa afya ya
uzazi,Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la kivulini mwanza Yassin Ally amesema
asilimia 60 ya wanawake hapa nchini wenye matatizo ya utoaji mimba hawapati
kabisa huduma ya matibabu wanayoyahitaji.
Marina Mashimba ni wakili wa
kujitegemea jijini Mwanza,anasema ili kupunguza au kuondoa kabisa vifo vya
akinamama na wasichana vitokanavyo na utoaji mimba usio salama,TAWLA imejikita
katika kupigania haki za wanawake na usawa wa kijinsia hapa nchini ikiwemo haki
ya afya ya uzazi katika kuleta maendeleo ya kiuchumi na kijamii pamoja na
kuondoa imani potofu kuhusu afya ya uzazi.
Mwaka 2007 Tanzania iliridhia mkataba wa nyongeza wa
haki za wanawake afrika ( Maputo Protocol ) wa mwaka 2003,ambapo katika ibara
ya 14 ( 2 ) ( c ), unatamka kuwa nchi wanachama zitachukua hatua madhubuti kulinda
haki za uzazi za wanawake kwa kuruhusu utoaji wa mimba pale ambapo mimba
imepatikana kwa ukatili wa kijinsia kubakwa,kufanya ngono maharimu au kama
kuendelea kukua kwa mimba hiyo kunahatarisha hali ya mama ya kiafya na kiakili
na mtoto aliye tumboni.
Source: ITV
Source: ITV
No comments:
Post a Comment