Rapper Kalapina ambaye amekuwa mstari wa mbele kusaidia baadhi ya watu
walioathirika na matumizi ya dawa za kulevya amemtaja mtu ambaye anasababisha
Chidi Benz asiachanwe na matumizi hayo.
Kalapina
amemtaja mama yake mzazi Chidi ndio anayesababisha rapper huyo asiachane na
matumizi ya dawa za kulevya kwa kuwa amekuwa akimdekeza sana.
“Kiukweli mama yake mzazi ChidI
Benz anampenda sana mwanaye na hali hiyo inampelekea mdogo wangu yule kuona
hata nikizingua mama atanitafuta tu, au kuona mama atasimama na yeye tu sababu
mama yake anampenda sana,” Kalapina amekiambia kipindi cha Planet Bongo cha EA
Radio.
“Siyo Chidi Benz tu wazazi wengi
wanawalea watoto kwa kuwadekeza sana. Wazazi hawana muda na watoto na hili
linachangia vijana kuingia kwenye madawa ya kulevya hata kwenye ushoga pia.
Lakini sisi wazazi wetu zamani ulikuwa ukizingua unapigwa sana hivyo lazima
utanyooka tu,” ameongeza.
No comments:
Post a Comment