Msanii wa muziki na mama wa watoto wawili, Snura Mushi ameibuka na
kuiomba Serikali iangalie uwezekano wa kupunguza gharama za kipimo cha vinasaba
(DNA) ili watu wa hali ya chini waweze kumudu.
Akiongea
na gazeti la Mwananchi, muimbaji huyo alidai kipimo hicho kikipatikana kwa
urahisi, kitasaidia kupunguza kesi za wanaume kutelekeza watoto na kukataa
mimba.
Nyota huyo alisema DNA ikiwa bei
nafuu hata watu wasiokuwa na uwezo watamudu kupima tofauti na ilivyo sasa
ambako wachache ndiyo hupima.
Sanjari na hilo, Snura alishauri
itungwe sheria ambayo itambana mwanamume aliyempa mimba mwanamke na kukataa
kulipia gharama za matunzo ya ujauzito.
“Ili kukomesha suala la kukataa
mimba naona itungwe sheria ambayo itamlazimisha mwanamume kulipia gharama zote
za matunzo endapo itakuja kuthibitika kisayansi kuwa mtoto ni wake. Kama
anakataa mimba wala asilazimishwe asainishwe na mwanamke asubiri
atakapojifungua ipimwe DNA, ikibainika kuwa mtoto ni wa mwanamume huyo atozwe
gharama zote alizotumia mama kulea ujauzito,” alisema msanii huyo ambaye mwaka
jana alifungiwa kutokana na video yake ya Chura kutozingatia maadili na sasa
amejikita zaidi kwenye muziki wa Singeli.
Muimbaji huyo kwa sasa anafanya
vizuri na video ya wimbo ‘Shindu’.
No comments:
Post a Comment