Katika muda ambao waigizaji wengi wa India kwa sasa wameelekeza macho
yao Hollywood, superstar Shah Rukh Khan ana mtazamo tofauti.
Yeye
anadai kuwa ataendelea kufanya filamu India hadi pale atakapotengeneza filamu
ambayo dunia nzima itaipenda. “Ndoto yangu siku zote imekuwa ni ndogo na ndoto
yangu ni kutengeneza filamu moja India ambayo dunia nzima itaipendda na kuwa
kubwa India. Kama nikiifanya kama mtayarishaji, muigizaji, mtu wa taa, au mtu
wa kamera, vyovyote vile, nataka tu kutengeneza filamu hiyo moja hapa India,”
SRK alisema kwenye mahojiano.
Alipoulizwa kuhusu Priyanka Chopra
na Deepika Padukone ambao tayari wameingia Hollywood, muigizaji huyo mwenye
miaka 51 alisema, “ni shukrani nyingi kwa Deepika na Priyanka, nadhani kwa
walichokifanya ni chachu kwa waigizaji wengi pia kwenda Hollywood.”
No comments:
Post a Comment