Wanawake wenye umri mkubwa wanaoishi bila kufanya mazoezi, wanazeeka haraka kuliko wale hufanya mazoezi kila siku.
Utafiti uliofanyiwa wanawake 1500 wenye umri wa kati ya miaka 64 na 95, uligundua kuwa wale waliotumia muda wao mwingi wakiwa wameketi na kufanya mazoezi yasiyozidi dakika 40 kwa siku, wana seli zenye umri miaka minane zaidi kibaolojia.
Wakati watu wanazidi kuwa na umri mkubwa, seli zao nazo huzeeka.
Watafiti kutoka Carlifonia wanasema kuwa watu wanastahili kufanya mazoezi hata wakati wa uzeeni na wazuie kuketi kwa zaidi ya masaa 10.
Watafiti hao wanasema kuwa wakati mtu anapozeeka seli ndogo kwenye DNA huwa fupi kimaumbileSeli zinazojulikana kama telomeres ndizo huzuia seli za DNA kuwa dhaifu.
Urefu wa Telomeres ndio huonyesha uzee wa mtu.
Kuendelea kuzeeka kwa seli za Telomeres, umehusishwa na hatari ya mtu kupatwa na mshutuko wa moyo na magonjwa kama kisukari na saratani.
Mozoezi yana manufaa
Utafiti uliofanywa na taasisi ya matibabu huko Carlifornia, uligundua kuwa wanawake ambao wanaketi kwa saa nyingi, hawangepatwa na kuzeeka kwa seli za Telomeres iwapo wangefanya mazoezi kwa takriban dakika 30 kwa siku.
Watu walio na umri mkubwa wanashauriwa kupunguza muda wao wa kuketi kwa sababu maisha kama hayo huchangia kuibuka kwa afya mbaya.
Utafiti huo pia unasema kuwa watu walio na umri wa zaidi ya miaka 65 na walio na afya nzuri, wanastahili kufanya mazoezi ya takriban dakika 150 kama vile ya kuendesha baiskeli, na kutembea kila wiki.
Pia watu hawa wanastahili kufanya mazoezi yanayoshirikisha viungo muhimu vya mwili kama vile miguu, mgongo, kifua, mikono na mabega kwa siku mbuli au zaidi kila wiki
No comments:
Post a Comment