Rais John Magufuli Ambaye ni Mwenyekiti
wa Taifa wa CCM, amesema ushindi wa CCM
wa ubunge na madiwani katika Uchaguzi Mdogo uliofanyika juzi nchini ni ishara
ya ushindi wa chama chake katika uchaguzi ujao kutokana na wananchi kuonesha
imani kwake na serikali yake.
Rais Magufuli aliyasema hayo kwa
waandishi wa habari muda mfupi kabla ya kumpokea Rais wa Uturuki, Recep Tayyip
Erdogan aliyefika Ikulu, Dar es Salaam jana akiwa kwenye ziara yake ya siku
mbili nchini.
Rais Magufuli alisema ushindi huo
ni kipimo cha utendaji wake kwa wananchi na hivyo umemuongezea ari ya
kuwatumikia wananchi kwa moyo wake bila ya kujali changamoto mbalimbali
zilizopo.
“CCM Oyee! Mnaonaje ushindi wa CCM?
Hii inadhihirisha ni namna gani wananchi walivyo na imani na mimi na serikali
yangu. Tumeshinda ushindi wa kishindo katika kata na Jimbo, wenyewe mmeshuhudia
namna tulivyowapiga. Au mnasemaje?” Rais Magufuli aliwaambia
waandishi wa habari na kisha akawashukuru na kuelekea eneo lake maalumu
akimsubiria Rais wa Uturuki kwa ajili ya kumpokea.
CCM mbali ya kushinda kiti cha
ubunge cha Dimani visiwani Zanzibar, imeshinda kata 18 kati ya kata 20
zilizofanya Uchaguzi Mdogo wa Udiwani juzi kutokana na sababu mbalimbali
zikiwamo za kufa kwa waliokuwa wakishikilia nyadhifa hizo na kufutwa kwa matokeo
kwa amri ya mahakama.
Kata ambazo CCM imeshinda ni
Nyarenanyuki (Arumeru, Arusha), Isegehe (Kahama, Shinyanga), Nkome (Geita),
Kiwanja cha Ndege (Manispaa Morogoro), Lembeni (Mwanga, Kilimanjaro), Ihumwa
(Dodoma), Matevez (Meru, Arusha), Kimwani (Muleba, Kagera), Igombavanu
(Iringa), Kijichi (Mbagala, Dar es Salaam), Ng’hambi (Dodoma), Kinampundu
(Singida), Kasansa (Katavi), Malya na Kahumulo (Mwanza), Mkoma (Mara),
Misugusugu (Kibaha, Pwani).
Aidha, CCM imeshindwa katika Kata
ya Duru mkoani Manyara, ambako mgombea wa Chadema, Ali Shaaban ameibuka
mshindi.
No comments:
Post a Comment