GARI LENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI 200 LATOLEWA KWA AJIRI YA KUBEBA WAGONJWA - OREST NGOWI

Breaking

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Monday, 27 February 2017

GARI LENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI 200 LATOLEWA KWA AJIRI YA KUBEBA WAGONJWA



Wanachi katika mamlaka ya mji mdogo wa katoro wilayani na mkoani Geita wameishukuru serikali kwa kuwapatia gari la kubeba wagonjwa  (ambulance ) lenye thamani ya shilingi milioni 200  kwa kupitia wizara ya afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto.


Gari hilo limekabidhiwa rasmi february 25 ,2017 katika kituo cha afya cha katoro ambapo viongozi mbalimbali wa kiserikali  wakiongozwa na mkuu wa wilaya ya geita mwalimu herman  kapufi pamoja na mbunge wa jimbo la busanda mh. lolencia  bukwimba walijitokeza katika tukio hilo .

Baadhi ya wananchi walio jitokeza katika tukio hilo  wamesema kuwa wanaishukuru serikali kwa jithada za makusudi  za kuwapelekea gari la wagonjwa  katika eneo hilo kwani mamlaka ya mji mdogo wa katoro una idadi kubwa ya watu ambao walihitaji  huduma ya gari la wagonjwa kama hilo kwa kufanya hivyo itasaidia kupunguza vifo visivyo kuwa  vya lazima ikiwa ni pamoja na  akina mama wajawazito na watoto.

Kwa upande wake mbunge wa jimbo  hilo  mh: lolencia bukwimba  ametumia fursa hiyo kuwa omba  kina mama wajawazito  kuhudhulia na kuzingatia ratiba ya clinic ili kuepuka madhara ambayo yanaweza kujitokeza   wakati wa kujifungua.  

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here