Wakazi katika kata ya buseresere wilayani chato mkoani Geita wameiomba serikari kuwa boreshea miundombinu ikiwa ni pamoja na mitalo ya
kusafirisha maji taka ili kuepuka kukumbwa na magonjwa ya mlipuko kutokana na
mvua za masika kuanza kunyesha.
Hatua hiyo imekuja baada ya mvua za masika kuanza kunyesha kwa
kasi katika eneo hilo jambo ambalo limesababisha maji kutuama katika makazi ya
watu kutokana na ujenzi holela huku watoto wadogo wakihofiwa kufa maji kutokana
na maji hayo kutuama katika mshimo ya taka yaliyopo karibu na makazi ya watu.
Wakizungumza na storm habari mapema hii leo kijijini hapo baadhi
ya wakazi katika eneo hilo wamesema kuwa wanaiomba serikali kuwaboreshea miundo
mbinu itakayo wezesha maji kuto tuama katika makazi ya watu kwani hali hiyo inakwamisha
shughuli za kiuchumi kutofanyika hasa vyumba vya kulala wageni kukosa wateja
kutokana na kujaa maji.
kwaupande wake mzee shaaban
abeid ambae ni mwenyeji wa eneo hilo na aliwahi kuwa afisa
mtendaji wa kata ya buseresere amesema kuwa madhara ambayo yanaweza kujtokeza
kutokana na maji kukosa njia ya kupitia ni pamoja na nyumba zao kubomoka hasa
kwa mvua zinazo nyesha nyakati za usiku.
Aidha afisa mtendaji wa kijiji cha buseresere bw issa muhamed husein amesema kuwa
kumekuwa na idadi kubwa ya nyumba ambazo zime jengwa kiholela katika eneo hilo
na ameiomba serikali kupitia halmashauri
ya wilaya ya chato kuboresha miundombinu ikiwa ni pamoja na kupanga kijiji
hicho ili kuondokana na adha kama hizo.
No comments:
Post a Comment