Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul
Makonda, amemkumbusha Spika wa Bunge. Job Ndugai, kuhusu kusudio lake la kuanza
kuwapima wabunge kubaini kama wametumia kilevi kabla hawajaiingia kwenye ukumbi
wa chombo hicho cha kutunga sheria.
Siku chache baada ya Rais Magufuli
kutengua uteuzi wa Charles Kitwanga, kwenye baraza lake la mawaziri kutokana na
kuingia bungeni akiwa amelewa, Ndugai alisema kuwa kuna wabunge kadhaa huingia
bungeni wakiwa wametumia vilevi vikali zaidi vikiwemo bangi, viroba na unga’
Aidha kutokana ba hatua hiyo, Spika
huyo alisema wanafikiria kuweka vifaa maalumu vya kupima ulevi kwa watunga
sheria hao na kutafuta wataalamu wa kutoa ushauri nasaha wa kisaikolojia,
utaratibu huo haujaanza kutolewa bungeni licha ya kwamba ni miezi tisa ipite,
Jana katika hafla maalum ya
kukabidhi orodha mpya ya watuhumiwa wa biashara haramu ya madawa ya kulevya
Kumkaribisha Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kupambana na Kuzui Dwa za Kulevya,
Rogers Siang’a, Makonda alimkumbusha Spika Ndugai kusudio lake la kuanzisha
utaratibu wa kuwapima wabunge ulevi.
“Na utaratibu huu wa kuwapima
wabunge wetu utakuwa mzuri sana, na ninakumbuka kuna kipindi Spika aliwahi
kutangaza kuanzisha lakini sijui ukaishia wapi, nitoe tena rai kwake afikirie
tena kuanzisha utaratibu huu ili tuweze kuwabaini wabunge kama wanatumia kilevi
ama la,”alisema Makonda.
No comments:
Post a Comment