Mtu
mmoja asiye tambulika kwa jina wala makazi na anaye kadiliwa kuwa na umri wa
kuanzia miaka 24 na kuendelea
amekutwa amefariki kandokando ya barabara iendayo shule ya sekondari lutozo
katika mamlaka ya mji mdogo wa katoro wilayani na mkoani geita .
Mwenyekiti
wa mtaa wa afya bw masaga misso ambapo mwili
huo umeonekana amesema kuwa tukio
hilo limetokea hapo jana majira ya saa kumi
na moja alfajiri ambapo mtu huyo
alishambuliwa na wananchi wenye hasira
kari kwa kusadikika kuwa ni mwizi wa
mahindi pamoja na mihogo mashambani.
Kwa
upande wake kamanda wa jeshi la jadi (sungusungu)
katika mtaa huo bw mashaka venas amewataka wananchi katika eneo hilo kuto
jijengea tabia ya kuchukua sheria mkononi pindi wamkamatapo mtu kwa tuhuma
yeyote.
Aidha
baadhi ya wakazi walio shuhudia mwili huo wamewataka vijana kuachana na tabia
ya wizi na badala yake wajishughulishe katika shughuli ndogongogo zinazo weza
kuwa patia kipato ambacho kina weza kuwaondoa katika mawazo mabaya kama ya
wizi,utumiaji wa madawa ya kulevya na
mambo mengine yafananayo na hayo.
No comments:
Post a Comment