Wazazi na walezi wa mtaa wa mwatulole kata ya buhalahala
katika halma shauri ya mji wa geita mkoani geita wameweka mapango mkakati wa
kuinua kiwango cha elimu katika kata hiyo kwa kuadhimia kuwashusha madarasa
wanafunzi ambao wataonekana hawana uwezo .mzuri wa kusoma na kuandika.
Hayo yamebainishwa katika kikao cha wazazi na walezi kilicho
fanyika katika shule ya msingi nguzo mbili ambapo wazazi hao wamekubaliana kwa
pamoja kuwarusha watoto wao ambao watagundulika hawana uwezo mzuri wa kusoma na
kuandika .
Wazazi hao wamesema watakuwa tayari kuchangia michango ya
maendeleo ya shule kwa hiari ili
kupunguza baadhi ya changamoto za
upungufu wa vyumba vya madarasa pamoja na miundo mbinu ya barabara
katika shule zilizopo katika kata hiyo.
Kwa upande wake mwalimu mkuu wa shule ya nguzo mbili Grace
jonh amesema kuwa kume kuwepo na idadi kubwa ya wanafunzi katika shule hiyo
ambao imefikia hatua ya darasa moja kukaliwa na wanafunzi 200 badala ya
wafunzi 45 jambo ambalo linawapa kazi
ngumu namna ya kuwafundisha .
Aidha mwenyeki wa mtaa wa matulole bw Charles fikiri amewaomba wakazi
katika eneo hilo washilikiane kwa pamoja
katika juhudi za kuinua kiwango cha elimu katika kata hiyo kwa kuchangia michango ya hiari kwa lengo la kuleta maendeleo ya shule za msingi katika eneo hilo kutokana na shule
hizo kuwa na idadi kubwa ya wanafunzi.
Hata hivyo kiongozi huyo amechangia mifuko 22 ya saruji
katika shule za msingi mwatulole pamoja na nguzo mbili ili kutoa hamasa kwa
wazi kuliona sula la uchangiaji katika sekta ya elimu ni lamuhimu.
No comments:
Post a Comment