Mfanyabiashara maarufu na
Mwenyekiti wa Club ya soka ya Yanga Yusuph Manji amekua akishikiliwa na Polisi
kituo cha kati Dar es salaam toka Alhamisi ya February 9 2017 baada ya kwenda
kuhojiwa kutokana na kutajwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda
kwenye orodha ya watu 65 kwenye sakata la dawa za kulevya.
Jana jioni Mfanyabiashara huyo
alichukuliwa na gari la kubebea Wagonjwa lenye namba za usajili za DFP na
alionekana akitembea na kuingia kwenye gari hilo (Land Cruise Nyeupe) yeye
mwenyewe bila kubebwa au kusaidiwa huku gari lake aina ya Range Rover
likitangulia mbele na watu wengine.
Baada ya gari hilo kumchukua
msafara huo ulikwenda moja kwa moja kwenye Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete
Muhimbili Dar es salaam ambako watu mbalimbali wanaosumbuliwa na moyo hupata matibabu.
Gari la wagonjwa
lililombeba Yusuf Manji na gari lake binafsi katika viunga vya Taasisi ya Moyo
ya Jakaya Kikwete (JKCI).
No comments:
Post a Comment