Baadhi ya wakazi wilayani chato mkoani geita wametakiwa kuboresha vyoo
vya asili kuwa vya kisasa kutokana na mvua za masika kuanza kunyesha ili
kuepuka vyoo hivyo kutitia na
kusababisha magojwa ya milipuko yanayo weza kujitokeza kutokana na uchafu wa
vyoo hivyo .
Rai hiyo imetolewa na mwenyekiti
wa kijiji cha mapinduzi bw kitute kalegea kijiji hapo ambapo amesema kuwa kuna idadi kubwa ya wakazi katika eneo hilo ambao wanatumia vyoo vya asili
ambavyo haviwezi kudumu kwa muda mrefu kutokana na miundo mbinu yake
kujengwa kwa kutumia udongo pamoja na miti.
Kalegea amewataka wananchi ambao hawa
vyoo katika kjijini hicho wachimbe
mara moja kwani kume kuwepo na
baadhi ya wakazi katika eneo hilo ambao
hawana vyoo katika familia zao na badala yake huduma hiyo huipata katika
vichaka vilivyo jiranai na nyumba zao jambo ambalo ni hatari kwa afya zao
pamoja na kijiji kizima kwa ujumla.
Aidha baadhi ya wakazi katika
kijiji hicho bw james peter na halima
shaabani wamesema kuwa
kumekuwepo na idadi kubwa ya watu ambao wanatumia vyoo vya asili jambo
ambalo ni hatari kutokana na vyoo hivyo
kutitia wakati wa mvua za masika zinapo anza kunyesha kitendo ambacho
kinawafanya watumiaji wa huduma hiyo kukosa sehemu rasmi ya kujisaidia na
badala yake wengine kutumia mifuko ya plasitiki
kwa kujikimu na mifuko hiyo mara nyingi hutupwa kando kando ya vyanzo vya maji pamoja na
barabara kitu ambacho kinaweza
kusababisha magonjwa ya milipuko kwa
baadhi ya wakazi katika kijiji hicho.
No comments:
Post a Comment